Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hadhrat Ayatullah Makarim Shirazi amejibu swali la kifiqhi kuhusu “hukumu ya kumfuata mwanafunzi wa dini aliyevaa kilemba mwanafunzi asiyevaa kilemba,” ambalo linawasilishwa kwenu kama ifuatavyo:
Hukumu ya kufuata mwanafunzi wa dini aliyevaa Kilemba kumfuata mwanafunzi wa dini asiyevaa kilemba
Swali:
Kufuata mwanafunzi wa dini aliyevaa vazi rasmi (yaani mwenye kilemba) kumfuata mwanafunzi mwenzake ambaye hajavaa kilemba, hukumu yake ni ipi?
Jawabu:
Muda wa kuwa mwanafunzi wa dini aliyevaa kilemba na mwenye sifa stahiki za kuongoza sala yupo, basi kumfuata mwanafunzi asiyevaa kilemba kuna walakini (ishkali).
Maoni yako